News and Events

Shindano la kufanya ziara ya Kitalii na TIMU YA CABBIES DO KILIMANJARO

Hamasisha Utalii wa ndani USHINDE ZAWADI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO
AU ZIARA YA MBUGA ZA WANYAMA PAMOJA NA TIMU YA CABBIES DO KILIMANJARO

MSHIRIKI
Mtanzania/Anayeishi Tanzania/Follower wa akaunti (@tz_unforgettable) katika mtandao wa “Instagram”
Umri wa miaka 18 hadi 35/Mwenye afya na akili timamu.

Watumishi au washirika wa taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii; Waajiriwa au watoa huduma katika sekta ya utalii na wanandoa,wapenzi, wanafamilia wa karibu au washirika wa biashara au
taasisi ziliotajwa hapo juu hawaruhusiwi kushiriki.

Bodi ya Utalii Tanzania, Hifadhi za Taifa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (ikiwa ni pamoja na wawakilishi wake walioidhinishwa) wana haki ya kuchunguza watumiaji na/au akaunti zenye
ulaghai, matusi , au tabia zisizoeleweka kwa hiari yao, ndani ya muda wa promosheni au baada ya washindi kuchaguliwa. Aidha, Taasisi tajwa zina haki, kwa hiyari yao, kumuondoa mshiriki bila
kutoa taarifa kwa mshiriki.


Maelezo zaidi - Bofya hapa kupakua Tangazo

Events / Fair Fees

Event Status: Open

Instagram_contest_-_PROMO

  • Google+
  • PrintFriendly

Join us on Social Media