Hifadhi ya Taifa Mahale

Hifadhi ya Taifa Mahale

Mahale inaundwa na vilima vilivyojipanga na kufunikwa na misitu minene ikiwa na jumla ya kilomita za mraba 1,613. Kama ilivyo hifadhi jirani ya kaskazini ya Gombe, hifadhi ya milima Mahale ni makazi ya jamii adimu zilizobakia za Sokwe duniani.

Katika hifadhi hii yenye misilu minene inayovuta mvua kwa wingi, kundi kubwa la Sokwe huonekana katika vilima na mabonde. Mabaki ya matunda yaliyoliwa pamoja na kinyesi kibichi ni mingoni mwa vitu vitakavyowaongoza wageni hadi kuwafikia viumbe hawa.

Eneo hili pia linajulikana kama Nkungwe, jina linalotokana na mlima mkubwa zaidi katika hifadhi hii. Ukiwa na urefu wa mita 2,460 ni mrefu zaidi ya vilele sita vinavyotengeneza safu ya milima ya Mahale inayokinga mitelemko yake katika Ziwa Tanganyika.

Hifadhi hii iko magharibi mwa Tanzania ikiwa inapakana na Ziwa Tanganyika.

Katika milima hii utaona sehemu ya asili ambayo watu wa kabila la Watongwe walikuwa wakiabudu mizimu yao milimani, kisha kurudi ziwani na kujitumbukiza katika maji baridi na maangavu ya ziwa Tanganyika lenye sifa ya kuwa na zaidi ya aina 250 za samaki.

Unaweza kufika katika Hifadhi hii kwa kupitia Kigoma ambako kuna meli au kwa ndege za kukodi au barabara kutoka Kigoma.

Wakati mzuri wakutembelea hifadhi hii ni kipindi cha kiangazi, kati ya Mei na Oktoba.

Kuna maeneo ya malazi yenye hadhi tofauti tofauti ndani ya hifadhi kama kambi za kifahari, nyumba za wageni na kambi za kupiga mahema.


Hifadhi ya Taifa Mahale Articles

0

Hifadhi ya Taifa Mahale Accommodations

0

Hifadhi ya Taifa Mahale Nearby Attractions

Hifadhi ya Taifa Gombe
Hifadhi ya Taifa Gombe, ni ndogo kuliko zote nchini ikiwa na jumla ya kilomita za mraba 52 tu, lakini ina umaarufu mkubwa unaotokana na kuwa na wanyama aina ya Sokwe.

Things to do:

Lake Tanganyika
Lake Tanganyika is the world’s longest (660km), deepest in Africa and second-deepest in the world (more than 1436m) and second-largest (by volume) freshwater lake. At somewhere between nine and 13 million…

Things to do:

Kigoma Town
The bustling town of Kigoma is the regional capital of western Tanzania and a central port in the area. Located on the eastern shores of Lake Tanganyika, Kigoma is surrounded by rugged mountains and forests…

Things to do:

Do you have listing / info to add?     Add here

Join us on Social Media