Hifadhi ya Taifa Milima ya Udzungwa

Hifadhi ya Taifa Milima ya Udzungwa

Hifadhi ya Taifa Milima ya Udzungwa, yenye ukubwa wa kilomita za mraba 1,990, ni hifadhi yenye hazina ya aina nyingi za mimea, ndege na wanyama ambazo hazipatikani sehemu nyingine duniani.

Kati ya aina sita za jamii ya nyani wanopatikana katika hifadhi hii, mbili hupatikana katika Hifadhi hii pekee; mbega mwekundu wa Iringa (Iringa red colobus Monkey) na “Sanje Crested mangabey” ambaye alikuwa hajulikani hadi mwaka 1979.

Aina nyingine nne za ndege ambao hazikuwa zikifahamika hadi katika miaka ya karibuni; chozi bawa jekundu (rufous-winged sunbrid) na jamii mpya kugunduliwa ya kwale Udzungwa (Patridge­like Francolin) zinafanya hifadhii hii kuwa ni moja ya makazi makuu na muhimu ya ndege-pori barani Afrika.

Kivutio kikubwa zaidi ni Mto Sanje ambao unatoa maporomoko ya maji yenye urefu wa mita zipatazo 170 yakianguka kupitia msituni na kutua mithin ya mianzo ya ukungu bondeni.

Aina ya ua la “African violet” vile vile linapatikana ndani ya hifadhi hii katikati ya miti mirefu inayofikia mita 30. Wanyama wengine wanaopatikana ndani ya hifadhi hii ni pamoja na simba, chui, nyati na tembo.

Hifadhi hii iko umbali wa kilometa zipatazo 350 kusini mwa Dar es Salaam, kilomita 65 kutoka Hifadhi ya Mikumi.

Kuna maeneo ya kupiga makambi ndani ya hifadhi pamoja na hoteli ya Twiga inayomilikiwa na shirika (TANAPA).

Pia nje ya hifadhi katika mji wa Mang’ula kuna aina mbalimbali za malazi.

In this section

Getting there

Best time to visit


Hifadhi ya Taifa Milima ya Udzungwa Articles

0

Hifadhi ya Taifa Milima ya Udzungwa Accommodations

0

Hifadhi ya Taifa Milima ya Udzungwa Nearby Attractions

Selous Game Reserve
Selous Game Reserve is Africa's largest game reserve and one of favourite game viewing areas in Africa. Covering 50,000 square kilometres, is amongst the largest protected areas in Africa and is relatively…

Things to do:

Hifadhi ya Taifa Mikumi
Hifadhi ya Taifa Mikumi, ni moja ya hifadhi kubwa na mashuhuri nchini. Eneo kuu na muhimu katika hifadhi hii ni uwanda wa mafuriko pamoja na safu za milima ambazo zinapakana na hifadhi hii. Mbuga za wazi…

Things to do:

Morogoro Town
Morogoro lies in the agricultural heartland of Tanzania, and is a centre of farming in the southern highlands. Tobacco is grown in the region and consolidated here before going to the market. In addition…

Things to do:

Do you have listing / info to add?     Add here

Join us on Social Media