Hifadhi ya Taifa Ruaha

Hifadhi ya Taifa Ruaha

Hifadhi ya Taifa Ruaha, yenye ukubwa wa kilomita za mraba 20,226 ndiyo Hifadhi kubwa kuliko zote nchini na ya pili kwa ukubwa katika Afrika baada ya Hifadhi ya Kafue iliyoko Zambia.

Hifadhi hii ni maarufu kwa wanyama aina ya kudu wakubwa na wadogo ambao hupatikana kwa wingi katika hifadhi hii. Ustawi wa hifadhi hii hutegemea, kwa kiasi kikubwa, mto Ruaha mkuu ambao ndio tegemeo kubwa kwa maji kipindi cha kiangazi. Aina mbalimbali za samaki, viboko na mamba hupatikana kwa wingi katika mto huu. Wanyama kama pofu na swala pala hunywa maji katika mto Ruaha mkuu ambao pia ni windo la wanyama wakali kama simba, chui, mbweha, fisi na mbwa mwitu.

Hifadhi hii ina idadi kubwa ya tembo wanaokusanyika katika eneo moja kuliko eneo lingine lolote Afrika mashariki. Pia Hifadhi hii ina sifa ya kuwa na aina za wanyama na mimea karibu yote inayopatikana katika nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika.

Ruaha ipo katikati ya Tanzania umbali wa kilomita 128 magharibi mwa mji wa Iringa na inafikika kwa urahisi kwa kutumia ndege za kukodi. Aidha hifadhi hii inafikika kwa magari wakati wote wa mwaka. Kutoka Dar es Salaam, (kilomita 625), Mikumi, Iringa na Arusha kupitia Dodoma.

Unapokuwa hifadhini unaweza kufanya safari za miguu porini, safari za magari kuangalia magofu maeneo ya kihistoria, kisima cha Mkwawa, milima ya Nyanywa, makaburi ya Chifu Mapenza wa wagogo yaliyopo ndani ya hifadhi yanayosadikiwa kuwa ni maskani ya watu wa kale katika kijiji cha Isimila umbali wa kilomita 120 kutoka Iringa mjini. Magofu haya ni miongoni mwa maeneo muhimu yenye historia ya kale barani Afrika.

Wakati mzuri wa kutembelea hifadhi hii kuangalia wanyama ni wakati wa kiangazi (kati ya Mei hadi Desemba); kuangalia ndege na maua wakati wa masika (Januari - Aprili).

Malazi katika Hifadhi hii ni pamoja na Hotel, kambi za wageni, maeneo ya kupiga kambi na nyumba za wageni. (Cottages)

In this section

Getting there

Best time to visit


Hifadhi ya Taifa Ruaha Articles

0

Hifadhi ya Taifa Ruaha Accommodations

0

Hifadhi ya Taifa Ruaha Nearby Attractions

Iringa Town
Located in the southern highlands of Tanzania, near the country’s legislative capital of Dodoma and the agricultural centre of Morogoro, Iringa is a pleasant small town and a focus of regional agriculture…

Things to do:

Mbomipa WMA
Neighbouring the Ruaha National Park, Mbomipa WMA is made up of land carved from 21 villages located in Idodi and Pawaga administrative wards in Iringa Rural District.

Things to do:

Do you have listing / info to add?     Add here

Join us on Social Media