Hifadhi ya Taifa Saanane

Hifadhi ya Taifa Saanane

Hifadhi tarajiwa Saanane, ilianzishwa kama bustani ya kwanza ya wanyama nchini mwaka 1964. Lengo la kuanzishwa kwake ilikuwa kuhamasisha uhifadhi na kuelimisha jamii.

Jina la hifadhi hii lililokana na mwanzilishi wa bustani aliyeitwa Saanane Chawandi.

Kati ya mwaka 1964 na 1966 wanyama mbalimbali walihamishiwa katika kisiwa hiki.

Wanyama hao ni pamoja na mbogo, digidigi, tembo, pofu, pundamilia, pongo, swala pala, ngiri, kima, twiga, nungunungu, mamba n.k

Wanyama wakali kama faru na mbogo walifungiwa na wanyama wapole waliachwa huru.

Bustani hii iligeuzwa kuwa pori la akiba (game reserve) mwaka 1991.

Muonekano wa Ziwa Victoria kutoka katika kisiwa cha Saanane ni kivutio kikubwa. Vilevile muonekano wa Kisiwa cha Saanane uwapo jijini Mwanza ni kivutio kingine kikubwa.

Hifadhi hii tarajiwa ina eneo la kilomita za mraba 0.5, na iko umbali wa km 2 kusini magharibi kutoka katikati ya jiji la Mwanza, katika Ghuba ya Ziwa Victoria.

Kisiwa cha Saanane kinafikika kwa boti ukiwa Mwanza. Mtu anaweza kufika Mwanza kwa gari, ndege ama treni na kutoka Mwanza mjini kutembea kwa miguu ama kwa gari hadi geti la kuingilia Hifadhini.

Shughuli za kufanya hifadhini Saanane ni pamoja na kuangalia wanyama, kukwea miamba, kutizama ndege, na safari za kutembea.Vilevile, kupiga makasia kwa kutumia boti za wenyeji inaruhusiwa kupitia kwa mawakala wa utalii.

Hifadhi hii tarajiwa inafikika wakati wowote wa mwaka.

In this section

Things to do

Getting there

Best time to visit


Hifadhi ya Taifa Saanane Articles

0

Hifadhi ya Taifa Saanane Accommodations

0

Hifadhi ya Taifa Saanane Nearby Attractions

Hifadhi ya Taifa Rubondo
Hifadhi ya Taifa Rubondo ni kisiwa kilichopo pembezoni mwa Ziwa Victoria, ziwa ambalo ni la pili kwa ukubwa duniani, likiwa linaziunganisha nchi tatu, Tanzania, Kenya na Uganda. Kikiundwa na mkusanyiko…

Things to do:

Lake Victoria
With a surface area of 68,800 sq km (26,600 sq mi), Lake Victoria is Africa’s largest lake. In addition, it's the largest tropical lake in the world, and the planet's second largest freshwater lake.…

Things to do:

Ukerewe Island
Ukerewe is the largest island in Lake Victoria and the largest inland island in Africa, with an area of approximately 530 km². Ukerewe Island is situated in the Ukerewe District, nearly 50 km north of…

Things to do:

Mwanza City
The city of Mwanza is the major Tanzanian port on Lake Victoria and a major centre of economic activities in the region. The lake borders the country’s East African neighbours – Uganda to the north…

Things to do:

Do you have listing / info to add?     Add here

Join us on Social Media