Hifadhi ya Taifa ya Serengeti

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti inayopita katika mikoa ya Arusha,Mwanza,Mara na Shinyanga ni eneo pekee duniani lenye kundi kubwa la wanyama wanaohama katika mfumo mzima wa mlishano.


Serengeti Wilderbeasts Migration Map

Inasemekena neno Serengeti linatokana na neno la kimasai la sirenget lenye maana ya uwanda mpana wa nyasi fupi,malisho mengi na maji ya kutosha pengine ndiyo maana hifadhi hiyo inapewa majina mengi kama vile lulu,bustani ya Afrika na Edeni ya Afrika kutokana na utajiri wa maliasili uliopo ndani ya hifadhi hii.

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti yenye ukubwa wa kilometa za mraba 14,763 ilianzishwa mwaka 1951, ni Hifadhi ya Taifa ya pili kwa ukubwa nchini ikitanguliwa na hifadhi ya Taifa ya Ruaha yenye ukubwa wa kilometa za mraba 20,226.

Umaarufu wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti unatokana na kuwa na misururu mirefu ya nyumbu wanaohama kwa makundi na kuvuka hata mpaka wa Tanzania hadi hifadhi ya wanyama pori ya Maasai Mara nchini Kenya ambapo takwimu za TANAPA zinaonyesha kuwa kila mwaka zaidi ya nyumbu milioni moja,pundamilia 200,000, swala tomi zaidi ya 300,000 na pofu 12,000 huunga misafara ya kutafuta malisho na maji.

“Hifadhi ya Taifa ya Serengeti huchukuliwa kama moja ya maajabu ya dunia kutokana na tendo la uhamaji wa nyumbu kutoka kusini hadi kaskazini na kurudi, tendo ambalo linafanyika mara moja tu kwa mwaka tendo hilo linaifanya hifadhi hii kuwa Eden ya Afrika na kupendwa kutembelewa na watu wengi ulimwenguni kote’’,alisema.

Licha ya nyumbu wanyama wengine maarufu walao nyama katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni chui na simba ambapo utafiti umebaini kuwa ukubwa wa hifadhi hii umesaidia kudumisha uhai wa wanyama waliokuwa katika hatari ya kutoweka kama vile faru weusi na duma.

In this section

Getting there

Best time to visit


Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Articles

The Great Serengeti Migration
The great Migration of the Serengeti is considered one of 'The Ten Wonders of The Natural World’, and one of the best events in Tanzania to witness. A truly awe-inspiring spectacle of life in an expansive…

Logo Not Available

Author:
Zina Dale

Category:
Articles

0

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Accommodations

0

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Nearby Attractions

Lake Victoria
With a surface area of 68,800 sq km (26,600 sq mi), Lake Victoria is Africa’s largest lake. In addition, it's the largest tropical lake in the world, and the planet's second largest freshwater lake.…

Things to do:

Musoma Town
It is located on the shores of Lake Victoria in the north of Tanzania, near the Kenyan border. The town offers much amusement to the passing visitors and is a point of cultural interest for people wanting…

Things to do:

Do you have listing / info to add?     Add here

Join us on Social Media