Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara

Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara

Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara ni maarufu sana nchini kwa simba wanaopanda miti. Umaarufu wa hifadhi ya Ziwa Manyara unaongezeka kila siku kutokana na kukua kwa utaiii wa ndani ambapo wananchi wengi kutoka mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania hupenda kutembelea hifadhi hii.


Manyara Nat. Park Map, Click to Expand

Hifadhi hii ipo ndani ya Bonde la Ufa ambalo kingo zake zinaongeza mandhari nzuri. Ziwa Manyara lililo ndani ya hifadhi ni kivutio kikubwa kwa watalii kutokana no wingi wa ndege aina ya korongo walio na mvuto mkubwa kwa kila mtu. Ndege hao huonekana kama pazia kubwa jeupe nyakati za mchana wanapokuwa ziwani wakijipatia chakula na mapumziko.

Vile vile, umaarufu wa Hifadhi hii unakua kila siku kutokana na wingi wa wageni wanaotoka nje ya nchi. Idadi kubwa ya wanafunzi kutoka shule mbali mbali nchini hutembelea hifadhi hii kujionea maajabu ya dunia hasa viumbe wa porini (wanyama, mimea na ndege). Wanyama wanaopatikana ndani ya hifadhi hii ni pamoja na simba, nyati, tembo, chui, pundamilia na wanyama wengine wanaokula majani. Hifadhi hii pia inasifika kwa wingi wa ndege hasa heroe, na mnandi ambao huonekana katika makundi makubwa na kufanya eneo hili la kitalii kuwa na aina 400 za ndege wanaovutia.

Chemchem za maji moto ni maajabu mengine ndani ya hifadhi hii. Maji hayo yanayo-bubujika kutoka ardhini huonekana yakitoa mvuke kama vile maji yanayochemka jikoni. Chemchem hizi za maji moto ya asili zimekuwa zikibubujika bila kukauka kwa kipindi cha mamilioni ya miaka.

Kuna maeneo ya malazi ndani ya Hifadhi yenye hadhi mbalimbali kama Hoteli za kitalii, nyumba za wageni na makambi ya kupiga mahema. Vilevile wageni wanaweza kupata malazi nje ya hifadhi katika mji mdogo wa Mto wa Mbu. Mji huu ni kituo kikubwa cha biashara kinachotoa huduma kwa wageni wanaotembelea hifadhi ya Ziwa Manyara. Unaweza kupata malazi na huduma za vinywaji katika mji wa Mto wa Mbu, baada au kabla ya kutembelea hifadhi ama nyakati za jioni.

Mji huu mdogo upo karibu na lango la hifadhi. Huduma zote muhimu zinapatikana hapa, jambo linaloifanya hifadhi ya Ziwa Manyara kuwa eneo pekee la kitalii

nchini Tanzania lililo rahisi kutembelewa na wananchi kwa gharama nafuu, hasa kwa sababu ya malazi na chakula ambayo hupatikana kirahisi na kwa bei ya kawaida katika mji wa Mto wa Mbu.

Hifadhi hii iko umbali wa kilometa 126 kutoka Arusha mjini, ina ukubwa wa kilomita za mraba 330.

Wakati mzuri wa kutembelea hifadhi hii ni kuanzia mwezi June hadi Desemba kabla ya mvua za masika.

In this section

Getting there

Best time to visit


Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara Articles

0

Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara Accommodations

0

Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara Nearby Attractions

Mount Ol doinyo Lengai
"Oldoinyo Lengai" means “The Mountain of God” in the Maasai language. The summit of this strato-volcano is 2962 metres above sea level, and affords direct views into the caldera of Tanzania’s only…

Things to do:

Hifadhi ya Taifa Arusha
Hifadhi ya Taifa Arusha, yenye ukubwa wa kilomita za mraba 328.4, iko umbali wa kilomita 62 (kiasi cha mwendo wa saa moja kwa gari) kutoka mji wa kitalii wa Arusha.

Things to do:

Lake Natron
A soda lake at the base of the active Ol Donyo Lengai volcano, the area around Lake Natron is often described as having a desolate and almost lunar beauty. Lake Natron is found in the northern part of…

Things to do:

Lake Eyasi
Lake Eyasi is a seasonal shallow endorheic salt lake on the floor of the Great Rift Valley at the base of the Serengeti Plateau, just south of the Serengeti National Park and immediately southwest of the…

Things to do:

Arusha City
Located in the northern highlands of Tanzania, beneath the twin peaks of Mt. Meru and Mount Kilimanjaro, Arusha is the safari capital of the country. Guests embarking on the popular northern safari circuit…

Things to do:

Do you have listing / info to add?     Add here

Join us on Social Media