Hifadhi ya Tarangire

Hifadhi ya Tarangire

Hifadhi ya Taifa Tarangire, yenye ukubwa wa kilomita za mraba 2,850, iko umbali wa kilomita 118 Kusini Magharibi mwa jiji la Arusha.


Tarangire Map, Click to Expand

Hifadhi hii ni maarufu kwa kuwa na makundi makubwa ya tembo wanaoweza kuonekana katika eneo dogo.

Tarangire pia ina mandhari nzuri ya kuvutia yanayo-tokana na maumbile ya mibuyu inayosadikiwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka elfu nane.

Wanyama wa aina nyingi wanaopatikana ndani ya hifadhi hii ni pamoja na pundamilia, nyumbu, swala, simba, nyati, kongoni, chui, duma na wengineo wengi.  Aina 550 za ndege hupatikana ndani ya hifadhi hii pia. Hifadhi hii ni maarufu katika ukanda wa kaskazini mwa Tanzania kutokana na wageni wengi, kutoka ndani na nje ya nchi, kupenda kutembelea hifadhi hii.

Umaarufu mwingine wa hifadhi hii ni pamoja na aina ya chatu walio na uwezo wa kukwea miti. Ni kutokana na umaarufu wa hifadhi hii idadi ya Watanzania wanaotembelea hifadhi hii imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.

Unaweza kutembelea hifadhi hii wakati wote wa mwaka na kuwaona wanyama wote bila matatizo kutokana na mazingira mazuri ya hifadhi yanayosaidiwa na Mto Tarangire unaokatiza katikati ya hifadhi.

Ndani ya hifadhi kuna nyumba za kulala wageni Hoteli za kitalii, maeneo ya kupiga mahema na kambi maalum kwa ajili ya watalii wanaotembelea hifadhi hii. Aidha malazi yanaweza kupatikana nje ya hifadhi.

In this section

Getting there

Best time to visit


Hifadhi ya Tarangire Articles

0

Hifadhi ya Tarangire Accommodations

0

Hifadhi ya Tarangire Nearby Attractions

Mount Ol doinyo Lengai
"Oldoinyo Lengai" means “The Mountain of God” in the Maasai language. The summit of this strato-volcano is 2962 metres above sea level, and affords direct views into the caldera of Tanzania’s only…

Things to do:

Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara
Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara ni maarufu sana nchini kwa simba wanaopanda miti. Umaarufu wa hifadhi ya Ziwa Manyara unaongezeka kila siku kutokana na kukua kwa utaiii wa ndani ambapo wananchi wengi kutoka…

Things to do:

Hifadhi ya Taifa Arusha
Hifadhi ya Taifa Arusha, yenye ukubwa wa kilomita za mraba 328.4, iko umbali wa kilomita 62 (kiasi cha mwendo wa saa moja kwa gari) kutoka mji wa kitalii wa Arusha.

Things to do:

Lake Natron
A soda lake at the base of the active Ol Donyo Lengai volcano, the area around Lake Natron is often described as having a desolate and almost lunar beauty. Lake Natron is found in the northern part of…

Things to do:

Lake Eyasi
Lake Eyasi is a seasonal shallow endorheic salt lake on the floor of the Great Rift Valley at the base of the Serengeti Plateau, just south of the Serengeti National Park and immediately southwest of the…

Things to do:

Arusha City
Located in the northern highlands of Tanzania, beneath the twin peaks of Mt. Meru and Mount Kilimanjaro, Arusha is the safari capital of the country. Guests embarking on the popular northern safari circuit…

Things to do:

Do you have listing / info to add?     Add here

Join us on Social Media