Hifadhi ya Taifa Mikumi

Hifadhi ya Taifa Mikumi

Hifadhi ya Taifa Mikumi, ni moja ya hifadhi kubwa na mashuhuri nchini. Eneo kuu na muhimu katika hifadhi hii ni uwanda wa mafuriko pamoja na safu za milima ambazo zinapakana na hifadhi hii. Mbuga za wazi ndizo zinashamiri katika uwanda wa mafuriko na kuishia katika misitu ya miombo inayofunika mabonde yaliyo chini ya hifadhi.


Mikumi Park Map, Click to Expand

Hapa simba wanao- nekana wakiwa katika himaya yao mara nyingine wakiwa juu ya matawi ya miti ili kukwepa majimaji wakati mvua zinapototesha ardhi ambayo ina udongo wa mfinyanzi.

Wanyama wengine wengi hukimbilia katika eneo la miombo nyakati za mvua ambako unaweza kuwaona kutoka eneo la safu za milima. Ni kutoka katika safu hii ya milima unaweza kuyaona makundi makubwa ya nyati katika uwanda huo wa miombo. Wakati wa mvua idadi ya ndege huongezeka na kufikia zaidi ya aina 300. Hii ni kutokana na ukweli kwamba nyakati hizi kunakuwepo makundi ya ndege wahamiaji kutoka nchi za Ulaya na Asia ambayo huungana na makundi ya ndege wakazi kama vile chole.

Vile vile makundi makubwa ya viboko, pundamilia na nyumbu yanaonekana katika eneo hili.

Hifadhi hii ina ukubwa wa kilomita za mraba 3,230 na ipo umbali wa kilomita 283 magharibi mwa Dar es Salaam.

Aidha hifadhi hii iko kaskazini mwa mbuga ya Selous na iko njiani unapoelekea au kutoka hifadhi za Udzungwa na Ruaha.

Unaweza kuunganisha safari ya hifadhi hii pamoja na hifadhi za Udzungwa, Selous na Ruaha kwa barabara kutoka Dar es Salaam. Hifadhi hufikika pia kwa ndege za kukodi kutoka Dar es salaam, Arusha na Selous.

Sehemu za malazi ni pamoja na hoteli za kitalii, nyumba za wageni hifadhini na maeneo ya kupiga makambi/mahema.

In this section

Getting there

Best time to visit


Hifadhi ya Taifa Mikumi Articles

0

Hifadhi ya Taifa Mikumi Accommodations

0

Hifadhi ya Taifa Mikumi Nearby Attractions

Selous Game Reserve
Selous Game Reserve is Africa's largest game reserve and one of favourite game viewing areas in Africa. Covering 50,000 square kilometres, is amongst the largest protected areas in Africa and is relatively…

Things to do:

Morogoro Town
Morogoro lies in the agricultural heartland of Tanzania, and is a centre of farming in the southern highlands. Tobacco is grown in the region and consolidated here before going to the market. In addition…

Things to do:

Do you have listing / info to add?     Add here

Join us on Social Media