Hifadhi ya Taifa Milima ya Udzungwa, yenye ukubwa wa kilomita za mraba 1,990, ni hifadhi yenye hazina ya aina nyingi za mimea, ndege na wanyama ambazo hazipatikani sehemu nyingine duniani.
Kati ya aina sita za jamii ya nyani wanopatikana katika hifadhi hii, mbili hupatikana katika Hifadhi hii pekee; mbega mwekundu wa Iringa (Iringa red colobus Monkey) na “Sanje Crested mangabey” ambaye alikuwa hajulikani hadi mwaka 1979.
Aina nyingine nne za ndege ambao hazikuwa zikifahamika hadi katika miaka ya karibuni; chozi bawa jekundu (rufous-winged sunbrid) na jamii mpya kugunduliwa ya kwale Udzungwa (Patridgelike Francolin) zinafanya hifadhii hii kuwa ni moja ya makazi makuu na muhimu ya ndege-pori barani Afrika.
Kivutio kikubwa zaidi ni Mto Sanje ambao unatoa maporomoko ya maji yenye urefu wa mita zipatazo 170 yakianguka kupitia msituni na kutua mithin ya mianzo ya ukungu bondeni.
Aina ya ua la “African violet” vile vile linapatikana ndani ya hifadhi hii katikati ya miti mirefu inayofikia mita 30. Wanyama wengine wanaopatikana ndani ya hifadhi hii ni pamoja na simba, chui, nyati na tembo.
Hifadhi hii iko umbali wa kilometa zipatazo 350 kusini mwa Dar es Salaam, kilomita 65 kutoka Hifadhi ya Mikumi.
Kuna maeneo ya kupiga makambi ndani ya hifadhi pamoja na hoteli ya Twiga inayomilikiwa na shirika (TANAPA).
Pia nje ya hifadhi katika mji wa Mang’ula kuna aina mbalimbali za malazi.